Serikali imetangaza nafasi za kazi zaidi ya 6,180 katika sekta ya afya nchini na kuwataka wananchi wenye sifa stahiki kuomba nafasi hizo ili kuweza kutatua changamoto ya upungufu wa watumishi katika vituo vya Afya, Zahanati na Hospitali za Wilaya.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo amesema watumishi hao wataajiliwa kabla ya mwaka kuisha na kuongeza kwamba lengo la serikali ni kuboresha sekta ya afya nchini.

 “Naomba niwataarifu kwamba serikali ofisi ya TAMISEMI imepata kibari cha kuajiri watumishi wapya 6,180, watumishi hawa tunatarajia kuwa ajiri hivi karibuni kabla ya mwaka huu kuisha kwa hiyo napenda kuutangazia umma kuwa dirisha la ajira lipo wazi, kwa watu wote wenye sifa kuhakikisha wanaomba nafasi hizo lengo kubwa ni kupata watumishi kwaajili ya vituo vya afya vipya tunavyovijenga”.

Waziri Jafo ameongeza kuwa watumishi waliokua wanajitolea watapewa kipaumbele zaidi, “kuna vijana wengine wamemaliza taaluma yao na hawataki ipotee wameamua kuomba nafasi mbalimabi kwa ajili ya kujipa uzoefu kwahiyo watu hao watakua kipaumbele chetu cha kwanza katika kuwaingiza katika ajira”.

Waziri wa Tamisemi amesema serikali inakamilisha ujenzi wa vituo vya afya 208 ambavyo vitagharimu shilingi bilioni 156 katika ujenzi wa miundombinu na vifaa tiba, pia serikali inajenga hospitali kubwa za wilaya takribani 68 na zitagharimu shilingi bilioni 105.

Watakaoajiriwa ni wenye sifa zifuatazo, Awe raia wa Tanzania, kuambatanisha nakala ya cheti cha kuzaliwa, kidato cha nne na sita, cheti cha taaluma na asiwe muajiliwa wa serikali au shirika la dini ambapo mshahara wake unalipwa na serikali, umri usizidi miaka 45 na utayali wa kufanyakazi mahali popote nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *