Lugha ya Kiswahili kimeweka historia yakuwa lugha ya kwanza kutambuliwa na mtandao wa kijamii wa Twitter.

 

Awali, Twitter ilikuwa ikiyatambua maneno ya Kiswahili kama maneno ya ki Indonesia katika swala zima la tafsiri.

 

Hata hivyo, mtandao huo sasa umeanza kuyatambua maneno ya Kiswahili na kutoa tafsiri inayoendana na lugha inayozungumzwa na kuandikwa sana Mashariki na Kusini mwa Afrika.

 

Takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa lugha hii inatumiwa na watu zaidi ya milioni 50 haswa katika maeneo ya Afrika Mashariki.

 

Vile vile, Kiswahili kimeorodheshwa kama lugha ya taifa kwa mataifa ya Tanzania, Kenya pamoja na Uganda.

 

Licha ya kutambulika, Kiswahili bado hakijaongezwa katika mtandao huo wa Twitter unaotumiwa Zaidi na viongozi duniani.

 

Tangu wiki iliyopita, Twitter ilianza kuyatmbua maneno ya Kiswahili na kuyapa tafsiri kama ilivyo kwa lugha nyingine za kigeni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *