Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Taifa (CHADEMA) Mhe, Freeman Mbowe amefunguka na kutoa neno kuhusu madiwani 46 ambao wamejiuzulu nafasi zao na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kusema kuwa jambo hilo linafanywa na CCM kwa lengo la kuwakatisha tamaa wana CHADEMA.

Mbowe amesema kuwa wapo watu wanadhani kitendo cha baadhi ya madiwani kuhama CHADEMA na kwenda CCM ni kukiuwa chama hicho na kusema suala hilo haliwezi kutokea kwani madiwani wa CHADEMA nchi nzima wapo zaidi ya 1130 huku madiwani 46 ndiyo waliohama na kwenda CCM.

Mbowe amesema kitendo hicho kinawapa funzo katika maandalizi ya kutafuta viongozi ambao kweli wanaweza kukisimamia chama na si wale wanaotafuta fursa za kutoka kupitia uongozi.

Mbowe amesema kuwa hao viongozi ambao wanahama kutoka CHADEMA na kwenda CCM kwao ni kama funzo kwamba wapo viongozi na watu mbalimbali ambao wapo ndani ya CHADEMA kwa lengo la kutafuta fursa tu na wanapoikosa hiyo fursa na ulaji wanaamua kuondoka.

Jumla ya madiwani 46 wamehama Chadema na kujiunga na CCM kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za maendeleo zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *