Mbunge wa Jimbo la Ulanga, Goodluck Mlinga, akichangia hoja katika bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani amelitaka Jeshi la Polisi chini ya IGP Simon Sirro kutumia mamlaka yake kisheria kuwadhibiti wanaoumtukana Rais na Amri Jeshi Mkuu wa nchi kupitia mitandaoni.
Mlinga ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma huku akitaja baadhi ya akaunti alizodai zinaongoza kuwatukana viongozi wakubwa wa nchi akiwemo Rais, mawaziri, wabunge na wananchi wengine wa kawaida.
Aidha, Mlinga amelitupia lawama jeshi hilo akidai limekuwa likiwanyima haki watuhumiwa kwa kuwabambikizia kesi, trafiki kuwakamata waendesha bodaboda na kuwatoza faini kubwa huku akidai pia kumekuwepo na kukithiri kwa vitendo ndani ya jeshi hilo.
Mbunge huyo amelitaka jeshi la Polisi kutumia nguvu zao katika kutatua tatizo hilo la matusi katika mitandao ya kijamii.