Mchezaji tenisi wa Uingereza, Andy Murray amefanikiwa kutetea taji lake la Olimpiki kwa upande wa wanaume baada ya kumfunga Juan Martin del Potro kwa seti nne katika mashindano ya Olimpiki mjini Rio.

Murray alishinda kwa seti  7-5 4-6 6-2 7-5 na kuibuka na medali ya dhahabu ambapo mpaka sasa timu ya wanamichezo kutoka Uingereza imetimiza medali 15 za dhahabu.

andy-murray-rio-2016-

Andy Murray anayeshika namba 2 kwa ubora dunia alimfunga mchezaji, Roger Federer na kushinda taji hilo katika mashindano ya Olimpiki yaliyofanyika jijini London mwaka 2012 ambapo sasa ametetea taji hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *