Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo, Joh Makini amefunguka kuhusu tetesi za kufanya kolabo na msanii Ice Prince kutokea Nigeria.
Joh Makini amesema ni kweli kuna kazi wamefanya pamoja ila hajapenda kuweka wazi hilo kwani yeye ndiye aliyetafutwa kwa ajili ya kolabo hiyo kama ilivyotokea kwa Davido.
“Kuna mtu mmoja anaitwa ‘Eze’ alikuja Bongo tukakutana akaniambia anafanya kazi na Ice Prince na ninadhani kuna kitu inabidi ufanye naye nikamwambia why not kwa sababu na mimi namkubali,” amesema Joh Makini.
Ameongeza kuwa siku iyofuata Ice Prince alimtumia wimbo pamoja na beat akaingiza verse yake kisha akamtumia hivyo hatua yoyote itakayofuata ni kutoka kwa msanii huyo na menejimenti yake.
Katika hatua nyingine amewajibu wale ambao wanadai kuwa kolabo yake na Davido haijawa kubwa kama ilivyotarajiwa.
“Mwisho wa siku nafanya muziki wangu kwani najua wapo watu wanaoupenda na wanaoamua kutokupenda, wanaweza kukukatisha tamaa, hao walikuwepo since day one kabla sijawa Joh Makini.