Muigizaji wa Bongo Movie, Aunty Ezekiel anatarajia kuzindua filamu yake mpya inayokwenda kwa ‘Mama’ ifikapo Mei 13 mwaka huu.
Aunty amesema kuwa changamoto alizokutana nazo kwenye chumba cha kujifungulia ndio sababu ya kutunga na kuandaa filamu ya ‘Mama’.
Pia amesema ameamua kuandaa filamu hiyo ili kuonyesha thamani ya mama na amepanga kuizindua kwenye Ukumbi wa Mlimani City.
Alisema lengo la filamu hiyo ni kuwafanya watu na jamii kwa ujumla kuona thamani ya mama na kuwaheshimu.
Aidha, alisema mama mara zote amekuwa na mchango mkubwa katika jamii huku akipambana zaidi na familia ikilinganishwa na kina baba.
Alisema katika movie hiyo ambayo ameifanyia katika Kijiji cha Kisarawe mkoani Pwani, ameshirikiana na mtoto wake (Cookie) na hakutaka kumshirikisha mumewe (Mose Iobo) kwa kuwa fani yake ni mnenguaji.