Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize amefunguka sababu ya kutompa mkono Alikiba walipokutana katika msiba wa Agness Masogange.

 

Harmonize amesema kuwa mambo yote yanayozungumzwa si ya kweli, bali walisalimiana ila si kwa kushikana mikono.

 

Amesema kuwa “Unajua asilimia kubwa ya watu wanaozungumza hawakuwa pale, unajua unapomzungumzia Alikiba ni mtu ambaye amefanya muziki wetu upate heshima kwa namna moja au nyingine, kama msanii namheshimu siwezi nikakutana na mtu halafu nisimsalimie, sio kweli,”.

 

Pia amesema kuwa “Kilichofanyika ni kwamba Diamond kamsalimia kwa mkono, wamesamiliana kwa mkono. Mimi nimekuja nimezunguka nikaona kwa kuwa Diamond kamsalimia kwa mkono, kamgeuzia kiganja, mimi nikamsalimia kwa sauti tu, tukakaa pale tukaendelea.”

Harmonize alikutana na Alikiba kwenye mazishi ya Agnes Masogange yaliyofanyika katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *