Wanamuziki nyota nchini Kenya, Jaguar na Prezzo wamemaliza bifu lao lililodumu miaka mingi miongoni mwa wawili hao.
Jaguar na Prezzo walikuwa na tofauti za muda mrefu baada ya kuingia kwenye bifu zito miaka mingi lakini sasa wameamua kumaliza tofauti zao.
Kupitia akaunti ya mtandao wa Instagram wa Jaguar ameandika kuwa ameamua kumaliza tofauti na Prezzo ili waendelee kufanya muziki na kuleta mafanikio kwenye industry ya Entertainment nchini Kenya.
Pia kupitia akaunti ya Prezzo nae ameandika kuwa sasa hakuna tofauti miongoni mwa wawili hao na wameamua kumaliza bifu lao ili waendeleza yaliyomema katika kazi zao za muziki nchini humo.
Jaguar na Prezzo walikuwa na bifu kwa muda mrefu kutokana na kazi zao za muziki nchini Kenya lakini sasa wamemaliza tofauti hizo.