Nafasi ya pili imeshikwa na Mmarekani, Justin Gatlin aliyetumia sekunde 9.89 na kushinda medali ya fedha huku nafasi ya tatu ikikamatwa na Mkanada, Andre de Grasse akitumia sekunde 9.91 na kushinda medali ya shaba.
Mjamaika, Usain Bolt amekuwa mwanaridha wa kwanza kushinda mataji matatu mfululizo ya mita 100 kwenye mashidano ya olimpiki baada ya kushinda medali ya dhahabu mjini Rio nchini Brazil.
Bolt mwenye umri wa maiaka 29 ametumia sekunde 9.81 na kufanikiwa kushinda taji hilo kama alivyofanya katika mashindano ya olimpiki yaliyofayika Beijing 2008 na London 2012.