Muigizaji na mchekeshaji mkongwe, Amri Athumani ‘King Majuto’, anawaomba wasanii na wadau wa sanaa kumsaidia kufanikisha matibabu yake ya nyonga.
Msanii huyo amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa huo kwa muda mrefu sasa na matibabu yake yanafanyika katika Hospitali ya Tumaini jijini Dar es Salaam.
Mzee Majuto ameomba kusaidiwa kufanikisha matibu yake kwa njia ya maombi pamoja na fedha kutoka kwa wadau wa Sanaa nchini.
Amesema kuwa “Watanzania waniombee niweze kurudi katika hali yangu, pia wanisaidie kukidhi gharama za matibabu, lakini kwa sasa hali yangu inaendelea vizuri,”.
Kwa upande wa mke wake, Aisha Yusuf amesema kuwa mume wake alifikishwa hospitali akiwa katika hali mbaya lakini anashukuru kwa sasa anaendelea vizuri.
Pia amesema kuwa Mzee Majuto amefanyiwa upasuaji wa pili kwa baada ya ule wa kwanza wa henia aliofanyiwa jijini Tanga Julai mwaka jana.