Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Linah Sanga amefunguka na kuwaambia wasanii wa kike kuwa ili kuendelea kimuziki inabdi wabadilike na kukubali changamoto ili kuweza kuendelea.
Linah amesema kuwa wasanii wengi wa kike wamekuwa na tabia ya kuogopa kuthubutu au kuwa na aibu ya kufanya kitu flani kwa kuhofia kuangaliwa wa jamii aua watu wanaomzunguka lakini ili kufanikiwa ni lazima kujitoa na kuji-brand ili kufanikiwa.
Linah anasema kuwa wasanii wengine wa kike wamekuwa wakitaka kukaa wao katika nafasi hizo, wamekuwa wanaoneana wivu kwa kushindwa kuwavuta au kuwaachia na wasichane wengien kuwa pale walipo wao.
Linah anasema kuwa wasanii wa kike inabidi waige mfano wa wasanii wkaubwa wa kike kutoka nje , hakuna madaraja ya msanii mkubwa wa kike kuliko mwingine na hiyo yote ni kwa sababu wamekuwa wakisaidiana na kuvutana kutoka chini.