Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amelihutubia Bunge la Afrika Mashariki mkoani Dodoma na kuwapongeza wabunge hao kwa kuchaguliwa kuwa wabunge wa Afrika Mashariki.

 

Rais Magufuli amewataka wabunge hao kuwatumikia wananchi wa Afrika Mashariki kwakuwa waliwachagua wakiwa na imani kuwa watawatumikia kwa uaminifu.

 

Amesema kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki imepiga hatua kubwa katika ukuaji wa uchumi duniani ambapo amewataka wabunge hao kushikamana ili kuweza kuimarisha uchumi zaidi.

 

Amesema kuwa Kwasasa tunaelekea hatua ya tatu ya ushirikiano wa kifedha, hivyo niwahakikishie kuwa tutafanya kazi kwa pamoja na nitawapa ushirikiano mkubwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *