Meneja wa muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu anayefahamika kwa jina la Neema Nepanya amesema kuwa Wema hakuhudhuria msiba wa Agness Masogange kwa kuwa alikuwa anaumwa tumbo.
Meneja huyo amefunguka hayo baada ya Wema kutoonekana kuhudhuria kwenye tukio la msiba wa Masogange.
Nepanya amesema kuwa “Wema alikuwa na nia ya kufika msibani kabisa na alikuwa ameshajiandaa lakini ilishindikana baada ya kuugua tumbo la ghafla ikabidi aahirishe tu, pia Mbeya alishindwa kusafiri maana Jumatatu ambayo ndiyo mazishi ya Masogange alikuwa anatakiwa kuhudhuria mahakamani kwenye kesi yake inayoendelea.
Awali habari zilidai kwamba Wema alishindwa kuhudhuria kwenye msiba huo kutokana na kwamba yeye na marehemu Masogange walikuwa na bifu kali na hawakuwahi kupatana.
Masogange alifariki dunia Aprili 20, mwaka huu katika Hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge jijini Dar na mwili wake kuagwa Aprili 22 katika Viwanja vya Leaders, Kinondoni na kusafirishwa nyumbani kwao Mbeya kwa mazishi yaliyofanyika Jumatatu iliyopita.