Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz jana amezindua wimbo wa maalumu kwa ajili ya kombe la dunia litakalofanyika nchini Urusi.
Wimbo huo uliotungwa na mwanamuziki Jason Derulo wa Florida, Marekani, Diamond ameshiriki kuweka maudhui ya lugha ya Kiswahili na umetayarishwa na prodyuza Nahreel kwa kushirikiana na maprodyuza kutoka nchi nyingine chini ya udhamini wa kampuni ya Coca-Cola.
Diamond amesema amefurahi kupata fursa ya kushiriki kuimba kuimba wimbo wa mashindano haya makubwa ya kidunia na kuitangaza Tanzania na lugha ya Afrika bila kusahau tasnia ya muziki kwa ujumla.
Kwa upande wake Meneja wa Chapa ya Coca-Cola nchini, Sialouise Shayo amesema kampuni ya Coca-Cola ambayo ni moja ya mdhamini wa mashindano haya makubwa ya soka duniani inayo furaha kwa msanii kutoka nchini Tanzania kushiriki kuimba wimbo maalum wa mashindano hayo.
Naye producer Nahreel ,ambaye ameshiriki kutengeneza wimbo huu aliishukuru kampuni ya Coca-Cola kwa jitihada mbalimali ambazo imekuwa ikifanya kuwanyanyua wasanii wa hapa nchini ambapo mbali na Diamond naye ameshiriki kwenye tukio hili kubwa.