Licha ya kisiwa cha Zanzibar kuwa na ardhi ndogo, huku pia ikiwa na mtaji na mapato midogo, imekuwa ikitumia mbinu mbalimbali kuhakikisha uchumi wake unaimarika.

Kwa mujibu wa Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar, Amina Salum Ali, uchumi wa Zanzibar sasa umekuwa kwa kwa asilimia 7.4 ingawa lengo kwa kipindi hiki ilikuwa kufikia asilimia 10, kuweza kufikia matarajio ya kuingia katika uchumi wakati, ifikapo mwaka 2020 na 2025.

Zanzibar imekuwa ikitegemea sana sekta ya utalii, Bahari na Kilimo katika kuimarisha uchumi wake.

 Akizungumza na BBC, Waziri Amina amesema wanaanza kuimarisha viwanda vya ndani kupitia sekta za kilimo, bahari na utalii kwa kuanza kufufua viwanda vilivyokufa kama vile vya chumvi.

Katika bajeti ya mwaka huu, Zanzibar imeanzisha wakala wa kushajihisha viwanda vidogo na vya kati, kutokana na kwamba Zanzibar ina wajasiriamali wadogo wengi.

Hali ambayo pia itaweza kuwajenga ili bidhaa zao ziwe na ubora na kukidhi viwango vya kimataifa.

 vijana ni pamoja na kukosa masoko, mitaji, ya elimu ya kufanya biashara pamoja na usafirishaji.

Licha ya kwamba wafanyabiashara wengi wa Zanzibar wanategemea sana soko la Tanzania bara, lakini serikali imekuwa ikiwashauri kuzalisha pia bidhaa ambazo zitakuwa na soko la kimataifa.

Akizungumzia mahusiano ya biashara kati ya Zanzibar na Tanzania bara, Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Amina Salim Ali amesema jitihada zaidi bado zinahitajika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *