Mchekeshaji maarufu Bongo, Amri Athuman maarufu Mzee Majuto, amelazwa tena katika Hospitali ya Tumaini jijini Dar es Salaam baada ya kuzidiwa.
Mke wa mwigizaji huyo, Aisha Yusufu, amesema kuwa mume wake walimpeleka hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu.
Aisha amesema kidonda alichofanyiwa upasuaji kimeleta shida, hivyo kumpeleka kwa ajili ya uangalizi zaidi.
Majuto alilazwa hospitalini hapo Januari mwaka huu na kufanyiwa upasuaji wa tezi dume na hali ilikuwa vizuri.