Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA ) imetoa muda wa wiki mbili kwa wamiliki wa mitandao ya kijamii ya ‘blogs’, tovuti na aina nyingine ya vyombo vya habari vinavyochapisha kwenye mtandao kujisajili nchini Tanzania.

Ikiwa sehemu ya usajili, wachapishaji wote kwenye mtandao kwa maandishi, video na sauti wanapaswa kulipia ada ya usajili huo kwa mwaka dola 1,000 ambayo ni sawa na Milioni mbili za Kitanzania.

Aidha wachapishaji wa mtandao huo wanatakiwa kuhakikisha wanakamilisha vigezo vyote ambavyo wanatakiwa kuainisha ikiwa ni pamoja kuweka mfumo wakukagua taarifa zisozoruhusiwa katika mitandao na kuweka rekodi ya watumiaji wote, vikiwemo vitambulisho vyao na anuani za wasambazaji wa intaneti.

Kufuatia agizo hilo, TCRA imesema kwa atakayekiuka vigezo na masharti hayo itamlazimu kulipa faini isiyopungua dola 2,000 ambayo ni sawa na Milioni 4 za kitanzania au kufungwa jela kwa muda usiopungua mwaka mmoja au kuchukuliwa adhabu zote kwa pamoja.

Uamuzi huu hii umekuja kwa lengo la kudhibiti maudhui mitandaoni ikiwa ni matakwa ya sheria mpya ambayo ilionekana kuwa na mkanganyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *