Baada ya kufunga ya ndoa, mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba amewashukuru watu wote waliompongeza baada ya kufunga ndoa leo jijini Mombasa.

Alikiba amesema kuwa ndoa yake imeisha salama na anamshukuru mungu kwa jambo hilo pamoja na ndugu, jamaa na marafiki ambao wamejitokeza kumsapoti kwenye tukio hilo kubwa muhimu katika maisha yake.

Amesema kuwa “Wanasemaga macho hayana pazia na moyo hauna macho, lakini mimi moyo wangu umenusa tu mpaka huku, sijaweza kuona lakini moyo wenyewe ndiyo umependa, nipo Tanzania, ningeonaje huku Kenya? Moyo ndiyo umependa.

Pia amesema kuwa “Nimejiona nimetimiza umri, ni wakati wangu kuwa na mke, maisha ndiyo haya haya kinachotakiwa ni kupigana nayo ili uweze kuishi vizuri’.

Alikiba na Amina wamefunga ndoa katika msikiti wa Ummul Kulthum, mjini Mombasa leo Asubuhi ambapo tukio hilo limeshuhudiwa pia na ndugu na marafiki zake wa karibu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *