Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema wale wote wanaosema kampeni yake ya kuwasaidia akina mama waliotelekezwa na watoto imevunja sheria, pengine wana watoto nje na wanaogopa kujitokeza.

Makonda ameyasema hayo leo Aprili 19, katika uzinduzi wa hospitali ya kisasa ya mama na mtoto iliyopo Chanika iliyojengwa kwa msaada wa Shirika Maendeleo la Kimataida la Korea (Koica).

Jana, Waziri wa Sheria na Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi  akiwa bungeni alisema kampeni hiyo inaweza kuleta hali ya sintofahamu na akabainisha kuwa inapaswa kufanyika faragha na sio kama inavyofanyika sasa.

Awali, Waziri wa Afya, Jinsia, Wanawake na Watoto,  Ummy Mwalimu alisema kampeni hiyo ni sahihi ila kasoro yake ni kutokuwa na faragha, lakini akasema kwa sasa inafanyika huku picha za watoto zikifichwa.

Aliyeibua hilo bungeni jana alikuwa ni mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga aliyehoji uhalali wa kampeni hiyo na akahoji kama haivunji sheria na kuwavunjia haki wanawake na watoto.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *