Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linashikiria hati ya kusafiria na simu ya mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz baada ya kusambaza video chafu mtandaoni.
Mwanamuziki huyo jana aliachiwa na dhamana baada ya kukamatwa kwa kosa hilo na kupelekwa kituo kikuu cha Polisi.
Siku ya jumapili usiku Diamond alisambaza video chafu za utupu akiwa na mzazi mwenzae, mwanamitindo Hamisa Mobeto.
Mbali na Diamond, wasanii wengine waliokamatwa na kuhojiwa na jeshi la Polisi ni mwanamuziki wa Bongo Fleva pamoja na Bilnass ambao wao pia walisambaza video chafu katika mitandao ya kijamii.
Nandy na Bilinass walihojiwa kutokana na video yao ya faragha huku Diamond naye akihojiwa kwa kusambaza video yake akiwa faragha na mama wa mtoto wake, Hamisa Mobetto.
Baada ya wasanii hao kukamatwa juzi, walitakiwa kwenda tena kuripoti jana na waliachiwa baada ya kudhaminiwa wakitakiwa kuripoti Aprili 20, mwaka huu huku hati za kusafiria na simu zao zikishikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi.