Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba anatarajia kufunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi Aminah Rikesh jijini Mombasa nchini Kenya siku Aprili 26 mwaka huu.
Alikiba na familia yake tayari wameshasafiri jijini Mombasa kwa ajili ya harusi hiyo na mpenzi wake huyo.
Tetesi za mwanamuziki huyo kuoa zilisambaa katika mitandao ya kijamii baada ya kwenda kuomba baraka kwa rais mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete.
Harusi hiyo pia inatarajiwa kuhudhuriwa na Gavana wa jimbo la Mombasa nchini Kenya, Hassan Joho ambaye ni rafiki wa karibu wa mwanamuziki huyo.
Baada ya kumaliza kwa ndoa hiyo nchini Kenya, Muimbaji huyo atafanya sherehe nyingine nchini Tanzania wiki moja baada ya ndoa ya awali.