Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Shilole amekanusha kuvujisha video ya utupu ya wanamuziki wenzake, Nandy na Bilnass.
Shilole amesema kwamba ahusiki na hajawahi kuona picha yoyote ya wawili hao wakiwa faragha.
Shilole amesema post aliyoweka insta kuhusu kuwa na picha za faragha za wawili hao alikuwa anatania, lakini ukweli ni kwamba hana picha yoyote na hajawahi kuona picha yoyote kabla.
Pia Shilole amesema ahusiki kwenye kuvujisha video hiyo, isipokuwa inawezekana kuna mtu alikuwa nayo akapata kisingizio baada ya Shilole kupost ili aonekane ni yeye aliyevujisha.
Hivi karibuni baada ya video ya utupu ya Nandy na Bill Nas kuvuja mtandaoni, watu wengi wamekuwa wakimtuhumu Shilole wakiamini ndiye kavujisha.