Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ametoa ripoti ya idadi ya familia alizoziunganisha na idadi ya watu ambao tayari wamekwisha hudumiwa kisheria.

Amesema mpaka sasa amesuluhisha kesi 205, na kesi hizo zimezaa matunda ambapo watoto 205 wamekubaliwa na wanahudumiwa na baba zao na mama zao kama ambavyo ilitakiwa kuwa mbali na idadi hiyo Makonda ametangaza kuwa ikiwa leo ni siku ya tano tangu kuanza kwa zoezi hilo ameshahudumia wanawake 4000 na bado zoezi linaendelea. 

Mbali na kuwa tayari amehudumia idadi hiyo ya kinamama, bado namba ya kinamama ambao hawajahudumiwa ni kubwa na hii inaonyesha ni jinsi gani siku hizi watoto wengi wanalelewa na mzazi mmoja hali ambayo siyo nzuri hasa katika kukuza maadili ya mtoto kutokana na kuwa mtoto anakuwa katika mazingira magumu sana, hivyo akifika umri anaoweza kujitegemea ni rahisi sana kujiingiza katika shughuli hatarishi.

Hata hivyo mbali na kutoa msaada wa kisheria kwa kinamama hao waliotelekezwa Makonda ameamua kumimina neema kwa watoto wao kwa kuwapatia bima ya Afya ya matibabu bure kwa mwaka mzima.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *