Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Bilnass amekanusha kutoka kimapenzi na mwanamuziki mwenzake, Nandy licha ya picha na video kusambaa mtandaoni wakiwa pamoja.

Bilnass amesema kuwa hana mahusiano ya kimapenzi na Nandy na picha zilizosambaa katika mitandao ya kijamii ni picha za muda mrefu sana ila jana ndiyo zimesambaa.

Bilnass ameamua kufunguka kuhusu picha hizo na kusema kuwa picha kati yake na Nandy zilipigwa siku nyingi tangu mwaka jana walipokuwa studio na kulikuwa na watu wengi  mahali walipkuwa wakipiga picha.

Pia amesema kuwa picha kama hizo zinaweza kupigwa na mtu yoyote  na kwa upande wake hakuwa na wasiwasi wowte alipokuwa akipiga picha hizo ila tu watu wamefikiria walivyofikiria.

Picha na video za wawili hao zimesambaa katika mitandao ya kijamii zikiwaonesha wakiwa pamoja faragha mpaka kupelekea kuzua gumzo kwa mashabiki wao.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *