Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee amefunguka na kusema kuwa hana mpango wa kwenda nje ya nchi kutengeneza video kwani hapa Bongo kuna madirector wakali.

Vanessa Mdee amefunguka na kudai kuwa kutokana na maprodyuza wa video za muziki kujitambua na kuanza kutengeneza kazi nzuri, hakuna haja ya kutoka nje kwa sasa.

Vanessa  ametambulisha  video yake ya wimbo namba tisa unaopatikana kwenye albamu yake hiyo uitwao Wet aliomshirikisha G Nako, aliongeza kwamba hata akiwa na hamu ya kufanya kazi na prodyuza wa nje atahakikisha anamleta Bongo ili ashirikiane na maprodyuza wa ndani kufanya kazi.

Ni kawaida kwa mastaa wengi wa Bongo kama Diamond, Alikiba, Vanessa, Navy Kenzo kwenda kutengeneza video zao nchi za nje kama South Africa ambazo wamedai kuna madirector wazuri kabisa wa video lakini hivi sasa tunajivunia na vya kwetu kama Vanessa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *