Muigizaji wa  wa Bongo Movie, Wastara Juma ameibuka na kueleza siri za kuachika kwa ndoa zake tatu.

Wastara alisema kuwa, siri kubwa ya ndoa zake kuvunjika ni kutokana na kukosekana kwa maelewano ndani ya nyumba na siyo kwamba huwa anapenda kuachika.

“Unajua kuna vitu ambavyo ningevikubali kuvifanya nilipokuwa ndani ya ndoa, ungekuta sasa hivi nimeshakufa hivyo kuolewa na kuachika siyo kupenda, bali nilishindwa kukubaliana na mambo ambayo nilikuwa ninalazimishwa kuyafanya,”.

Wastara aliwataka wamama hao kuwa na ujasiri wa kufanya kazi kwa bidii na wasinyong’onyee kwa sababu ya kuwa wanawalea watoto peke yao baada ya kuzalishwa na wanaume kuwakimbia au kuachika katika ndoa.

Pia muigizaji huyo amewatia moyo wanawake wote wanaolewa watoto bila sapoti ya baba kuwa wavumilivu na kujituma ili kufanikisha ndoto watoto wao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *