Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka baadhi ya Wabunge Bungeni kuacha kuwatetea wasanii wanaoimba nyimbo zisizokuwa na maadili.

Waziri Mwakyembe ametoa kauli hiyo leo kwenye mkutano wa 11 kikao cha sita kinachoendelea kufanyika mkoani Dodoma wakati akijibu swali la Nyongeza kutoka kwa Mbunge Catherine Magige.

Mbunge Magige alitaka kufahamu ni kwanini kamati ya maudhui inashindwa kufanya kazi zake kwa wakati mpaka inafikia muda wasanii wanaachia kazi zao za sanaa ndio wao wanaibuka na kuanza kuwafungia kazi hizo, je wameshindwa kazi.

Pamoja na hayo, Waziri Mwakyembe ameendelea kwa kusema kwa kutumia baadhi ya nukuu ya Hayati Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere kwamba “Taifa lisilokuwa na utamaduni wake ni taifa mfu’. Sisi hatuwezi kukubali kuwa taifa mfu. Yanayotokea Tanzania yanatokea duniani kote”.

Kwa upande mwingine, Waziri Mwakyembe amesema Wizara yake kupitia kamati ya maudhui itaendelea kuzifungia nyimbo zisizokuwa na maadili ili waweze kulinda utamaduni wa taifa la Tanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *