Video vixen Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ amesema kuwa baada ya kesi yake kumalizika kwasasa hataki kabisa ukaribu na mtu yoyote.

Masogange alihukumiwa miaka mitatu au kulipa faini ya shilingi milioni 1.5 ambayo alifanikiwa kuilipa na kuepuka kwenda jela.

Masogange amesema kuwa, kwa sasa anataka aishi maisha yake ya kawaida na wala hataki kujihusisha na mambo ya kwenye mitandao ya kijamii kama ilivyokuwa mwanzo maana anaona hayo ndiyo yaliyomu-ingiza kwenye misukosuko.

Amesema  “Sasa hivi nataka kuishi maisha yangu ya kawaida kabisa, sitaki tena kujihusisha na mambo ya mitandao, nataka maisha yangu yawe ya kawaida kabisa“.

Agnes alikamatwa mwaka jana Kwa Tuhuma za kujihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya na mkemia mkuu wa serikali alithibitisha hayo baada ya kumpima.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *