Muigizaji wa filamu nchini India, Salman Khan amepata dhamana ya kifungo chake alichohukumiwa juzi.

Ikiwa ni siku tatu tangu mahakama nchini India kumhukumu kifungo cha miaka mitano jela kwa kosa la ujangili alilolifanya mwaka 1998, kwa kuua wanyama wawili jamii ya swala.

Mahakama mjini Jodhpur ilimpa hukumu ya miaka mitano jela pamoja na kumtoza faini ya dola $154 sawa tsh 347  kwa kosa hilo.

Maamuzi ya dhamana yametangazwa jana na Mahakama hiyo baada ya kundi kubwa la mashabiki wake kufurika katika gereza alilofungwa, mahakama hiyo ilimpa dhamana mkongwe huyo wa filamu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *