Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee amekumbwa na skendo ya utapeli baada ya watu waliouza albamu yake ya ‘Money Mondays’ kudai hawajalipwa pesa zao.

Watu hao wamesema kuwa hadi sasa hawalipwa pesa zao licha ya kusamba albamu ya mwanamuzki huyo.

Mmoja wa watu hao aliyefahamika kwa jina la Jacky Tarimo aliyedai kuwa wamefanya kazi ya kuuza albamu hiyo kwa siku ishirini lakini wakiombwa walipwe wanakataa.

Dada huyo amedai kuwa walikuwa wanataka  kufanya kazi mara mbili kwa wiki na kila siku ni shilingi elfu 15 na walifanya kazi kwa siku 15 lakini hawajaliowa hata senti mpaka muda huu.

Mwezi uliopita Vanessa Mdee aliachia albamu yake ya kwanza alioyoiita jina la Money Mondays.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *