Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize amefunguka na kusema kuwa anayaheshimu maamuzi ya Zari The Boss Lady baada ya kuamua kuachana na Diamond.

Kauli hiyo ya Diamond inakuja kufuatia kuulizwa swali iwapo amepokeleaje uamuzi wa mwanadada huyo.

Harmonize amesema kuwa anaheshimu maamuzi ya Zari kwa kuwa ana sababu zake za msingi kwani ni mtu mzima hawezi akakurupuka na kuamua kuandika ujumbe kama ule wa kuachana.

Pia amesema kuwa kwa upande wake hawezi kuingilia maamuziki ya mtu kwani kila mmoja ana uhuru wa kufanya akipendacho.

Katika siku ya wapendanao Zari The Boss Lady ambaye ni mzazi mwenzie na  Diamond Platnumz, aliposti Ua Jeusi katika mtandao wa Instagram na kutangaza kuachana kimahusiano na msanii huyo rasmi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *