Uongozi wa Jeshi la China umeahidi kuisaidia na kuiunga mkono Urusi kijeshi kukabiliana na mataifa ya Magharibi dhidi ya mzozo wa kidiplomasia, vikwazo vya kiuchumi na mazoezi ya kijeshi.
Ahadi hiyo imetolewa Waziri wa Ulinzi wa China, Wei Feng ambaye yuko Urusi kuhudhuria mkutano wa saba wa kimataifa wa usalama wa Moscow akiwa ameambata na ujumbe wa maofisa wa ngazi za juu wa jeshi.
Feng alisisitiza kwamba ziara yake imeratibiwa moja kwa moja na Rais wa China, Xi Jinping.
Alisema alikwenda Moscow akiwa na ujumbe maalumu kutoka kwa Jinping katika kipindi hiki ambacho mataifa yote mawili yanaboresha majeshi yao na ushawishi wao duniani licha ya wasiwasi wa Marekani.
Hali hiyo inakuja huku mataifa hayo mawili yakiingia katika mzozo na Marekani katika maeneo tofauti kuanzia kijeshi hadi kiuchumi.