Msanii wa hip hop Bongo, Roma Mkatoliki leo amesajili na kukabidhiwa rasmi cheti cha kutambulika na Baraza la sanaa la Taifa (BASATA).

Roma amekabidhiwa cheti na katibu mkuu wa Baraza la Sanaa nchini, Godfrey Mngereza katika ofisi za Baraza hilo zilizopo Ilala jijini Dar es Salaam.

Hii ni baada ya kupewa sharti na Wizara ya Habari ya kujisajili kwanza Basata ili aondolewe adhabu yake ya kufungiwa miezi 6.

Wizara ya habari utamaduni na michezo chini ya waziri wake, Dkt. George Mwakyembe ilimtaka Roma kujisajiri upya na kutambuliwa katika kazi zake za Sanaa.

Roma alifungiwa na wizara ya Habari, Sanaa, Utamudi na Michezo kutokana na nyimbo zake kutozingatia maadili katika jamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *