Mkali wa michano Bongo, Nikki Mbishi amefunguka na kuwapa pongezi uongozi wa WCB baada ya kufungua Wasafi Tv na kuanza kupiga nyimbo za wasanii tofauti.

Nikki Mbishi amesema alichofurahishwa zaidi na kituo hicho ni kwamba kimeanza kwa kupiga nyimbo mchanganyiko na bila ubaguzi kitu ambacho kinapelekea ushindani wenye usawa ambao awali haukuwepo kwenye media nyingine.

“Asante Wasafi TV nyie mmecheza wimbo wangu #NIMEKUMISS bila hata mimi kuwaletea, najua ndio mnaanza ila msisahau kuendelea hivi hivi. Hakuna kitu kinachojenga na kuimarisha misingi ya sanaa kama ushindani wenye usawa “Fair Competition” hii inamaanisha anayestahili na apate na asiyestahili akose japo fitna zipo tu,“ameandika Nikki Mbishi kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuelezea zengwe zilizokuwa zinafanywa na vituo vingine.

“Tumeshuhudia umwinyi na ubeberu kwa kipindi kirefu sana,wapo ambao walitaka uMungu mtu lakini walijishtukia wakabwaga na wengine walibwagwa na hiyo ni kwa sababu ya kuleta umatabaka wa kanda fulani na kanda fulani na kujuanajuana sana kiasi kwamba akina sisi tusiofungamana nao tukaishia kutengwa na kuonekana “VINEGA” Kila la kheri kwenye hii ligi ya mbuzi kuna siku daraja litapanda tutacheza ya ng’ombe na mpaka tembo nini simba. Ipo siku watajihoji na kujijibu wenyewe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *