Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dk Fidelice Mafumiko  kuwa Mkemia Mkuu wa Serikali.

Uteuzi huo wa Dk Mafumiko umeanza jana Jumanne Aprili 3, 2018.

Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu,  Gerson Msigwa imeeleza kuwa kabla ya uteuzi huo, Dk Mafumiko alikuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW).

Dk Mafumiko anachukua nafasi ya Profesa Samuel Manyele ambaye amemaliza muda wake katika kazi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *