Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametoa taarifa rasmi juu ya mazishi ya Winnie Mandela ambaye Taifa hilo linamtambua kama mama wa Taifa, aliyefariki April 1, mwaka huu.
Rais Ramaphosa amesema Winnie Mandela atazikwa kwa heshima zote za serikali na utamaduni wa Afrika Kusini hapo April 14, huku zikitanguliwa na shughuli zingine za mazishi kuanzia April 11.
Rais Ramaphosa ameendelea kwa kusema kwamba kama Taifa linatambua mchango wa Winnie Mandela, hivyo watampa heshima zote pamoja na watu wote wanaowatakia mema taifa la Afrika Kusini.
Winnie Mandela alikuwa mke wa pili wa aliyekuwa Rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, na alikuwa ni mmoja wa wapigania uhuru wa watu weusi na kuendeleza harakati hata wakati viongozi wa ANC akiwemo Nelson Mandela wakiwa wamefungwa jela, kwa muda wa miaka 27.