Video Queen Bongo, Agnes Gerald maarufu kama ‘Masogange’ amehukumiwa kwenda jela au kulipa faini ya shilingi milioni 1.5.

Masogange amekutwa na hatia na mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kwa kosa la kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin.

Masogange  alikuwa anakabiliwa na kesi ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepam, katika utetezi wake amedai kuwa yeye hajawahi kutumia dawa za kulevya hata siku moja.

Alidai kuwa Februari 14,2017 polisi walienda nyumbani kwake, yeye hakuwepo, alikuwepo dada yake, yeye alikuwa amempeleka mjomba wake kununua vitu Ocadeco.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *