Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Timbulo amewaomba radhi mashabiki wake kwa kitendo chake cha kukataa kutoa msaada kwa aliyekuwa mcheza shoo wake anayefahamika kwa jina la ‘Emma’.
Timbulo amesema kuwa nia yake haikuwa hivyo kwasababu hakuwaamini watangazaji wa kipindi cha Shilawadu waliompigia simu kuhusu suala la ugonjwa wa mcheza shoo huyo.
Mcheza shoo huyo amabe hali yake inaonekana kuwa mbaya sana kiafya amethibitisha kuumwa kwa muda mrefu sasa akisumbuliwa na kifua kikuu.
Emaa amesema kuwa amefanya kazi na wasanii wengi akiwemo Alikiba ambae ndie amekuwa msanii anaemsaidia na kumpa ela mara kwa mara kwa ajili ya matibabu lakini hawa wengine wamekuwa wakimkwepesha na hata kumkatia simu zake.
Wasanii waliowahi kufanya kazi na Emma ni Matonya, Alikiba, Timbulo, Nuh Mziwanda, Shilole, Dully Sykes, Queen Darleen, Rich Mavoko, Msaga Sumu, Sam wa Ukweli na Tunda Man.