Mke wa zamani wa Nelson Mandela, Winnie Mandela ambaye pia alipigana dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini amefariki dunia akiwa na miaka 81.

Winnie alizaliwa mnamo 26 Oktoba mwaka 1936, na ingawa yeye na mumewe – Nelson Mandela – walitalikiana mapema miaka ya 1990, Winnie Madikizela Mandela kama alivyofahamika rasmi alisalia kutoa mchango katika maisha ya Mandela.

Alikuwepo na walishikana mikono alipokuwa akiondoka gerezani baada ya kufungwa kwa miaka 27.

Msemaji wa familia Victor Dlamini amesema kupitia taarifa kuwa: “Amefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu, ambapo amekuwa akiingia na kutoka hospitalini mara kwa mara tangu mwanzo wa mwaka.

Askofu mstaafu na mshindi wa tuzo ya Nobel Desmond Tutu amemsifu kama “ishara kuu ya vita dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Alisomea kazi ya utoaji huduma za kijamii na haraka aliyazoea maisha ya kuwa mama na mwanasiasa.

Katika kipindi chote cha miaka 27 mumewe alipokuwa gerezani bila matumaini ya kuachiwa huru kutokana na hukumu ya kifungo cha maisha jela alichopewa mwaka 1964, Bi Winnie alilazimika kubeba jukumu la ulezi wa watoto na pia kuendeleza kampeni za kisiasa kutaka mashujaa wa kupigania nchi yao waachiwe huru hasa mumewe.

Kutokana na hayo Bi Winnie Mandela alilazimishwa kusalia tu huko Brandford katika jimbo lao la Orange Free katika miaka ya 70 baada ya operesheni mojawapo za kupambana na ubaguzi wa rangi zilizokuja kujulikana zaidi kama the Soweto Uprising.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *