Muigizaji nyota wa Bongo Movie, Aunty Ezekiel amekanusha taariza zilizoenea katika mitandao ya kijamii kuwa anaazimana nguo na rafiki yake Wema Sepetu.
Aunty amadai kuwa nguo inayodaiwa kuazimwa na Wema ni sare ambayo walishona siku moja ila yeye akavaa kabla ya mwenzake.
Aunty alisema kuwa nguo hiyo ambayo Wema aliivaa juzikati kwenye ‘bethidei’ ya Martin Kadinda walizishona sare ila yeye akavaa kwenye msiba wa bibi yake mwaka jana, hivyo kuwafanya watu wahisi Wema kamuazima.
“Kwanza kuazimana nguo sioni kama ni shida kwa sababu ni rafiki yangu lakini nguo wanayozungumzia zimefanana na wala hakuna aliyeenda kugonga hodi kwa mwenzake’.
Hivi karibuni wadau wa kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram, walitupia picha ya Aunt akiwa msibani akiaga mwili wa marehemu bibi yake huku akiwa amevaa gauni jeusi na upande mwingine Wema akiwa kwenye sherehe ya Kadinda akiwa amevaa gauni kama lilelile, jambo lililoibua madai kuwa, wana yale mambo ya kizamani ya kuazimana nguo.