Muigizaji wa Bongo Movie, Faiza Ally ameonyesha kuchukizwa na kitendo cha kampuni ya Soft Care inayojihusisha na utengezaji wa Pampas za watoto kumpa ubalozi, Zari The Boss Lady.
Kauli ya mwanadada huyo imekuja siku moja baada ya kampuni hiyo kumtangaza Zari kuwa balozi wa kutangaza bidhaa hizo nchini.
Faiza amesema kuwa ameshangazwa sana na kitendo hiko kwakuwa wapo watanzania wanaoweza kuwa mabalozi siyo mpaka kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kumchukua mtu kuwa balozi wakati amezidiwa umaarufu na baadhi ya mastaa wa Bongo.
Kupitia akaunti yake ya Instagram Faiza Ally amefunguka ‘
I know this is gonna look bad for somepeople but let me be honest , how stupid Tanzanian can be , mastaa wote watanzania , watu wote watanzania hamkuona hata mmoja anae stahili kupata dili zaidi ya zari ? Ina maana uhitaji bongo umeisha mpaka tuweke watu kutoka nje ?? Kwa nini tunawapa kipa umbele wageni tunajizarau sisi ??? Mlishawahi kuona Uganda na kenya wamempa nani dili wakamuacha wa kwao ?? Eti sasa hivi mganda na mkenya wanapongezan na sisi wote tunaonekana hatukufaaa.
Jana kampuni ya Soft Care ilimtangaza Zari The Boss Lady kuwa balozi rasmi wa bidhaa hiyo kwenye hafla iliyofanyika katika hoteli ya New African Hotel jijini Dar es Salaam.