Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amefunguka na kumtaka Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mohammed Mpinga kuunda kamati maalumu kuchunguza juu ya kifo cha utata cha kijana, Alen Achiles (20) aliyefariki muda mfupi baada ya kutoka mikononi mwa Polisi.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya alisema hayo kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Mbeya ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, William Ntinika ambaye alimuwakilisha kwenye msiba huo baada ya RC kupata dharura.
“Kutokana na tukio hilo RC amemuagiza RPC aunde kikosi kazi kitakachochunguza tukio hili toka lilipoanza mpaka tukio lilipofika mwisho na taarifa amkabidhi na wale watakaobanika kama mjuavyo nchi yetu inaongozwa kwa sheria hatua zitachukuliwa mara moja, hayo maagizo nimepewa kwa hiyo RPC naomba nifikishe ujumbe huu nilikuwa sijakwambia kwamba unaunda timu itakayochunguza ikiwashirikisha pia wanafamilia na jamii kwa ujumla ambayo inafahamu”.
Hata hivyo wananchi mbalimbali ambao walikuwepo eneo la msiba wameendelea kulinyooshea mkono jeshi la polisi kuhusika na kifo cha kijana huyo licha ya kuwa RPC mkoa wa Mbey alisema jeshi la polisi haliusiki na kofo cha kijana huyo na kudai kuwa aliondoka katika mikono yao akiwa salama.