Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe na viongozi wengine wa chama hicho, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kusomewa mashtaka yanayowakabili.
Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Habari CHADEMA Tumaini Makene amethibitisha hilo na kusema kuwa viongozi hao wamefikishwa mahakamani leo.
Viongozi wa CHADEMA wengine waliofikishwa Mahakamani ni Katibu Mkuu Dr. Vincent Mashinji, Mbunge wa Kibamba John Mnyika.
Wengine ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalim, Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa na Mbunge Ester Matiko.