Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewasimamisha kazi wakurugenzi wawili wa halmashauri za Kigoma Ujiji, Boniface Nyambe na Daud Mlahagwa (Pangani).
Rais Magufuli ametoa uamuzi huo leo baada ya kupokea ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad iliyobaini madudu katika ukaguzi wa serikali za mitaa na mashirika ya umma.
Akiwasilisha ripoti hiyo, Profesa Assad amesema serikali za mitaa 140 zilishindwa kukusanya mapato ya Sh116 bilioni ambayo ni sawa na asilimia 22 ya mapato yake.
Madudu mengine aliyobaini CAG ni kupotea kwa vitabu 379 vya mapato ya Serikali, ambavyo haikujulikana ni kiwango gani cha fedha kilichopotea kutokana na upotevu wa vitabu hivyo.
“Kitabu cha mapato kisipokuja kwetu hatuwezi kujua ni kiwango gani kimetumika katika vitabu hivyo, lakini tuliona katika halmashauri za Bihalamuro, Karagwe na Mpwapwa, kulikuwa na miradi mitatu ambayo thamani yake ilifikia Sh1.6 bilioni iliyocheleweshwa kukamilishwa.