Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amefanya mazungumzo ya siri na Baraza la Sanaa Taifa ‘BASATA’ baada ya kujibizana na Naibu Waziri wa Habari, Juliana Shonza.
Diamond alifika katika viwanja vya basata majira ya nchana akiwa na meneja wake, Sallam SK lakini mazungumzo yao hayakuwekwa wazi.
Muimbaji huyo alifika katika taasisi hiyo ya malezi ya wasanii kwaajili ya kuzungumza na viongozi hao juu ya kauli zake ambazo amekuwa akizitoa juu ya Naibu waziri huyo.
Hata hivyo Basata hawajatoa taarifa yoyote juu ya kikao hicho cha siri ambacho kilichukua masaa kadhaa.
Mapema wiki hii muimbaji huyo wakati anahojiwa na kituo cha redio cha Times FM aliitupia lawama Basata pamoja na Naibu waziri huyo baada ya kufungia nyimbo 15 za wasanii wa bongofleva zikiwemo zake mbili.
Kauli hizo zilimfanya Waziri wa Habari, Dk Mwakyembe kutoa kauli yake na kudai kwamba ameshtushwa na kauli za muimbaji huyo juu ya waziri.