Mwanamuziki wa Nigeria, Wizkid ameeleza jinsi alivyogeuza ujio wa mwanaye wa tatu kuwa siri kubwa kwa wazazi wake.
Wizkid amesema kuwa wazazi wake waligundua amepata mtoto wa tatu kupitia mitandao ya kijamii.
Amesema kuwa kitu cha ajabu ni hiki cha mwisho. Wazazi wangu waligundua nimepata mtoto wa tatu kwa kuangalia mtandaoni.
Pia ameongeza kwa kusema kuwa mama yake anataka sasa hivi ajipange ili afunge ndoa na akae na mwanamke mmoja na azae watoto.
Msanii huyo mwenye watoto watatu wa kiume ambaye kwake suala la kuwa na mke mmoja bado ni kitendawili alisema kuwa ana mpango wa kuongeza mtoto mmoja na anaomba awe wa kike.
Katika hatua nyingine, Wizkid alieleza kuwa kuna nyimbo mpya ziko jikoni ambazo ni moto wa kuotea mbali. Alisema kati ya nyimbo hizo, ipo aliyomshirikisha rapa wa kike Nicki Minaj.