Mwanamuzi wa hip hop, Roma Mkatoliki amelitaka Baraza la Sanaa nchini (BASATA) kumpunguzia adhabu ya kutojihusisha na muziki.
Basata wamesema walimfungia msanii huyo baada ya kutakiwa na baraza hilo kubadili wimbo huo lakini hakufanya hivyo na kila alivyoita hakuweza kutokea.
Roma amesema anawaomba BASATA kumpungia adhabu kwani hali yake ya kiuchumi siyo nzuri kutokana na kukosa show.
Amesema kuwa “Haya yote yanaongeleka, lengo ni Roma aendelee kufanya muziki wake kwa sababu muziki unamsaidia kama ajira, nyuma ya Roma kuna watu ambao anawasaidia. Kwahiyo wakati mwingine naomba ieleweke kwamba tufanye tu Roma aendelee na muziki wake ili maisha yake yaendelee,.
Pia ameongeza kwa kusema kuwa ”Tena nikitoka hapa nitawasiliana na Katibu mkuu wa Basata najua atanisikiliza, pia nimesikia Jumatatu kuna mkutano wa wasanii wote na BASATA utafanyikia pale BASATA, zote ni katika njia ya kwenda kuyaongelea haya mambo, lengo tuwe chombo kimoja.