Kesi inayomkabili video vixen Bongo, Agnes Masogange imeendelea tena leo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Kesi hiyo imesikilizwa leo majira ya asubuhi katika Mahakama hiyo ambapo Masogange anakabiliwa na mashtaka ya utumiaji wa madawa ya kulevya.

Mahakama hiyo imeahirisha kesi hiyo kutokana na wakili wake Ruben Simwanza kudai mteja wake huyo amelazwa katika hospitali moja hapa jijini Dar es salaam.

Hakimu ambaye anasikiliza kesi hiyo, Willbard Mashauri ametaja tarehe nyingine itakayoendelea kesi hiyo ambayo ni April 4 ya mwaka huu.

Masogange anatuhumiwa kwa kesi ya utumiaji wa madawa ya kulevya baada ya kutiwa hatiani mwaka jana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *