Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amepiga marufuku kukamatwa wasanii pindi wanapokuwa wanapiga picha au kuigiza katika maeneo ya bandari yanayoonesha taswira ya Jiji inavyoonekana kiujumla kwa madai kitendo hicho wanalitalitangaza kitalii.
Makonda ametoa kauli wakati wa ghafla ya uzinduzi wa kazi za kutangaza utalii katika Jiji la Dar es Salaam na kusema amepata malalamiko mengi kuhusiana na wasanii wanaokamatwa na wakiwa wapo katika shughuli za kuutangaza kiutalii mkoa wake.
Aidha, Makonda amesema wasanii hao hao wakienda kuigiza katika maeneo machafu huwa hakuna mtu anayejitokeza kuwakamata au hata kuwazuia jambo ambalo lina mkera kwa upande wake.
Pamoja na hayo, Makonda ameendelea kwa kusema “leo hii Ikulu ya Marekani ‘White House’ inajulikana kutokana na muvi zao wengine hatujawahi kutembelea baadhi ya nchini lakini ukiangalia ‘movie’ unaambiwa ndio sehemu fulani unakubali kumbe hata wakati mwingine unadanganywa”.
Kwa upande mwingine, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema inapaswa ifike wakati wasanii waliopo nchini Tanzania hasa katika jiji lake wawe wanarekodi kazi za kwa uhuru bila ya kupatiwa shida ya aina yeyote ile.